Wednesday, October 21, 2009

YALIYOJIRI

Naacha muziki - Chid Benz
Msanii anayebamba zaidi ktk muziki wa Hiphop nchini hivi sasa Chid bez ametangaz akuacha muziki kwa kile alichosema hawezi kuwa mtu wa kuomba msamaha kila siku na watu wakamuelewa.




Chid amezungukwa na utata ktk siku za karibuni baada ya kuripotiwa kumpiga msanii mwenzake Matonya wakati wa tamasha lililofanyika mjini Dodoma.

Rapa huyo wa ilala amesema amefikia uamuzi wa kuachana na muziki kutokana na matatizo yanayomwandama ...huku akigoma kueleza undani wa tukio la kumpiga Matonya.

"Naheshimu kazi yangu, naheshimu mashabiki wangu. Sina ubavu wa kulielezea kila jambo, ila ki-ukweli! ushindani UpO kwa sisi wasanii. Na kwa kazi yetu lazima kuwe na maneno mengi. Siwezi kuomba msamaha kila siku, najua nazidi kuwaudhi mashabiki wangu. Na kiukweli niko juu (hivyo) kila mwenzangu kazini anafurahia ninapopatwa na matatizo kama haya."

..."Mashabiki wasini-judge (wasinihukumu) vibaya.....Waamini kuwa hata rais
wetu (Jakaya Kikwete) anayependwa sana, toka awe madarakani amekuwa
akipata matatizo mengi nafikiri kuliko rais yeyote aliyewahi kuwa madarakani."

"Kuna mengi yanatokea katika hiili game lakini nafikiri ya kwangu
yamekuwa na bahati ya kusemwa hadharani japo sio makubwa sana ila yanaendana na nilivyo kwa sasa."

"Nashukuru kuna watu hawachoki kunipa sapoti...naheshimu leo....Nafikiria Fiesta ya Dar Nov 8 kama nitaruhusiwa kufanya onyesho ndio itakuwa show yangu ya mwisho.

Tukio dhidi ya Matonya ni la pili ktk miezi michache baada ya hivi karibuni kufikia kuomba msamaha hadharani kufuatia tukio lililoripotiwa sana la kumpiga Prof Jay.



Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

2 comments:

  1. Ebwanae,dah pole sn kwa matatizo yanayokukumba bro.Unajua nilitaka kukuuliza sababu iliyofanya usi perform kwenye fiest lkn nilikuwa nasahau but now i know.Ila mi nadhani matatizo ni sehemu ya maisha ya binadam na kuyakabili matatizo ni moja ya vipimo vya mwanaume kamili.Lakini pia bro kumbuka kuwa hakuna kazi ambayo haina misukosuko na ukiwa ni m2 wa kukata tamaa kila matatizo yanapokukuta utabadilisha kazi nyingi sana.Ninachoweza kukushauri mimi ni kwamba we kaza buti komaa na wala usifikirie kuacha mziki kwani kwa muda mfupi 2 ambao umefanya mziki umeweza kujikusanyia kundi kubwa la mashabiki wa mziki huu wa bongo.Ningekushauri pia km unaona ni ngumu sn kutuomba tena msamaha mashabiki basi angalau kaa chini na uyamalize na hao wasanii wenzako ambao umegombana nao.Ni hayo 2 bro..,Pole sana.Naitwa Nurudin Zuber ni rafiki yako pia kwenye facebook so tunaweza kuwasiliana.

    ReplyDelete
  2. mweshimia king sisi apa nimashabiki wako wa buja bwiza nasisi nima lafamilia soldier tunakuomba usiacilie kamba w njo captain wa meli kubwa tunakubali salut...jeyamafia lafamilia&babuji sylla&luendo aire&mwamedi couture&fiston malikiti&havana club

    ReplyDelete